DRCongo

Mashriki Ya Kiraia Kutoka Wilaya Ya Nyiragongo,Rutshuru Na Masisi Yaomba Wanajeshi Wote Kuondoka Katika Mji Wa Goma Na Kwenda Kwenye Uwanja Wa Mapigano.

Aprili 15, 2024
Border
news image

Katika mkutano na wanahabari wilayani Nyiragongo leo hii juma tatu tarehe kumi na tano elfu mbili ishirini nan ne Mashirika ya kiraia toka wilaya tatu yaani Nyiragongo ,Rutshuru na Masisi yaomba kamanda wote wa jeshi la Congo kuondoka katika hoteli za Kifahari Mjini Goma na kwenda kwenye uwanja wa mapigano ,hii itarahisisha Mji wa Goma kuwa na usalama na kupunguza idadi kubwa na wanajeshi wanao sababisha ukosefu wa usalama asema MAMBO KAWAYA.

Kawaya amesema wazalendo kama vile wanajeshi wote lazima kupelekwa kwenye uwanja wa mapigano kuliko kubaki mjini kuhangaika na silaha mikono ,ikiwa chanzo cha ukosefu wa usalama na kushindwa kufahamu nani mwanajeshi nani M23 ,Kawaya ameongeza kuwa haijaelekweka kuona wanajeshi walio kuja kupugana kulala katika hoteli japo mwanajeshi apashwa baki kwenye musatari wa mapigano.

Leopoled MUISHA kutoka shirika za kiraia katika Mji wa Sake wilayani Masisi kwa upande asema hali kwa wakimbizi ni mbaya hasa wakishuhudia makombora katika kambi za wakimbizi,nakuona wanajeshi wanakaa kimia kuliko kushughulikia swala la usalama na kuwarudisha nyumbani wakimbizi wa vita wanao patikana katika baadhi ya kambi bila msaada na wengi wakianza kupoteza Maisha kutoka na njaa kubwa kambini.

Mashirika ya kiraia ikomba wapiganaji walendo kuheshimu sheria za taifa na kuwalinda wananchi ambao ni ndugu zao ,Mapigani kati ya waasi wa M23 na serikali ya Congo imesbabisha janga kubwa la kiutu mashariki mwa Congo ,hali bado ikienelea kuwa mbaya Zaidi.

AM/MTV DRC ONLINE